Msanii Adekunle Gold kutoka Nigeria na Belle 9 kutoka Tanzania

Belle 9 ni miongoni mwa wasanii wa mda mrefu na ambao wamekomaa kwenye game mpaka sasa na anafanya vizuri na hit song yake Give It To Me.

Kutana na Belle 9 kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo.
 
Hit maker huyu kwa sasa hivi ameweza kuingia studio na msanii kutoka nchini Nigeria anayefahamika kama Adekunle Gold.
 
 
Imetajwa kuwa tayari wameshaingia studio na wimbo huo umebeba tittle ya Tutafutane.
 
Staa huyo wa Nigeria chini ya label ya YBNL inayomilikiwa na Olamide amesema kuwa Belle 9 ndiye msanii wa kwanza kukutana naye na kurekodi. 
 
Belle 9 alipoulizwa experience yake ilikuaje na msanii huyo kutoka Nigeria alisikika akijibu, "Adekunle Gold ni mtu mzuri sana."