Rapper wa Tanzania AY

Kutana na rapper huyu mkongwe kutoka Tanzania AY ambaye kwa sasa hivi anahit na ngoma yake mpya More ambayo ni collabo ameifanya na Nyashinski wa 254 Kenya.

Burudika na hit hii ya More kwenye Mziki Fresh, Jumatano saa 18:00 kwenye Trace Mziki (323).

Rapper huyu ni miongoni mwa wasanii wa kwanza kufanya collabo na wasanii wa Marekani akiwemo Romeo, L’amyia na Sean Kingston. Na sasa hivi anakuja kivingine tena ndani ya 2017, tutarajie collabo kati yake na Busta Rhymes.
 

Kwa mujibu wa rapper huyo mkongwe AY, meneja wake wa Marekani Hemdee ndiye anayeweka mipango sawa ya kufanyika kwa wimbo huo.

“Hemdee bado anaendelea kuishughulikia hiyo kazi na mwaka huu tunaweza kuwa na rekodi moja na Busta Rhymes,” AY alieleza

“Bado hatujaanza kurekodi lakini bado tunaendelea kuumiza kichwa tujue beat ni ya aina gani, tufanyaje sisi na yeye.”

Mengi ya marapper kutoka Tanzania, Mwana FA amewaambia nini mafans wake? Soma yote hapa.