Msanii Chege Chigunda kutoka Tanzania

Leo kutana na Chege Chigunda msanii  kutoka Tanzania ambae anafanya vizuri kwenye game tangu kitambo ambae pia yupo kwenye kundi la wanaume family TMK.

Mwimbaji huyo ambaye hivi karibuni ameachia wimbo mpya Kelele za Chura akiwa amemshirikisha Nandy, amedai suala la kuoana linakuja kutoka kwa Mungu na sio kuigana.

Mengi ya mapenzi na ndoa, uliyaskia ya Diamond na Zari kupata shavu kwenye jarida la Mamas and Papas kule Afrika Kusini?

“Mimi siwezi kuoa sijui kwa sababu nikienda kwenye interview nitaulizwa, mbona wewe haujaoa, mbona mwenzako kaoa. Siwezi kuoa kwa sababu Mh Temba kaoa,” Chege alisema
 
Alimalizia, “Mimi nitaoa pindi tu mwenyezi Mungu atakaposema Chege oa lakini sio kwa sababu fulani kafanya hivyo."
 
Labda Chege hayupo tayari kufunga ndoa, lakini kutana na wapenzi kutoka Tanzania na safari yao ya harusi na ndoa kwenye Harusi Yetu, Jumamosi saa 17:00 ndani ya Maisha Magic Bongo .