Tanzanian artist Chaz Baba

Chaz amethibitisha kwamba yuko studio na anarekodi album ya nyimbo zake kwani anataka kuipeleka pakubwa dance ya Tanzania kama anavyofanya Diamond Platnumz nje ya mipaka ya Tanzania.

Kutana na staa wa muziki wa dance Tanzania Chaz Baba ambaye alichukua headlines za kutosha mwaka juzi pale aliposajiliwa na Band ya Mashujaa kwa mkataba aliouita mnono ikiwemo kulipiwa kodi ya nyumba.

Kwenye exclusive interview na dstv.com Chaz ambaye kwa sasa bado yuko na Band ya Mashujaa amesema anafurahia kuwepo hapo japo haimaanishi atakaa hapo milele.
 
Amesema hawezi kuahidi kwamba hiyo ndio itakua ni band yake milele, huu ni muziki na soko linabadilika so usishangae ukamuona kahamia sehemu nyingine sababu mwisho wa siku bado anatafuta pesa.
 
Kwenye headline nyingine, Chaz amethibitisha kwamba yuko studio na anarekodi album ya nyimbo zake kwani anataka kuipeleka pakubwa dance ya Tanzania kama anavyofanya Diamond Platnumz nje ya mipaka ya Tanzania.
 
Kuongea kuhusu Diamond, je umempigia kura katika tuzo za MTV Africa Music Awards 2015?  Kaka yetu ameteuliwa katika category: Best Male, Best Collaboration kwa nyimbo wa Bum Bum akimshiriki Iyanya wa Nigeria na  Best Live. Mpigie kura hapa kaka Diamond. Kisha ungoje kutazama tuzo hiyo live kutoka mjini Durban Jumamosi 18 July saa 21:00 CAT kwenye MTV Base.