Producer Lizer wa WCB

Inawezekana ukawa umekutana na jina la Lizer (Sirajy khamis Amani) kwenye nyimbo nyingi za wasanii waliopo kwenye label ya WCB ya msanii Diamond Platnumz. Lizer amekuwa kati ya producers ambao wasanii wengi wanatamani kufanya naye kazi kutokana na kazi zake kusifika ndani na nje ya Tanzania.
 
Katika stori tulizopiga na Lizer, aligusia changamoto anazokutana nazo ndani ya kuwa producer wa studio ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platnumz.
 
Kuburudika na hits kutoka WCB, tazama Mziki Hit 10, kila Ijumaa saa 17:15 ndani ya TRACE Mziki (323).
 
Inafahamika kuwa kumekuwa na ushindani wa kibiashara kati ya Diamond na Alikiba ambao wengine pia huita bifu ambalo limekuwa likiendelea kwa muda,
 
Lizer ameelezea hii imemfanya baadhi ya watu ambao sio mashabiki wa Diamond kumdhania kuwa hawezi kufanya kazi na wasanii wengine zaidi ya wale wa WCB pia hata mitaani wakati mwingine anakutana na changamoto za watu wa namna hiyo  kujiepusha naye kwa kumuita timu Diamond .
 
Lizer amesema, "Watu hawajui kuwa mimi nafanya kazi na kila mtu na sifanyi kazi kwenye label ya WCB peke yake huwa nashangaa baadhi ya watu wanapokuwa na wasiwasi kufanya kazi na mimi, ndio nipo WCB ila hiyo hainifanyi nione wengine sio bora."