Msanii wa bongofleva Tanzania Gentriez

DStv inakuletea msanii kutoka bongoflevani Gentriez ambaye ameongelea changamoto alizozipata wakati anatoka kimziki pale anapopeleka video zake kwenye vituo vya televisheni na radio.

Msanii Emmanuel Mwakitabu anafahamika kama Gentriez Tanzania ambae ni mmiliki wa hit single ya Chapaa Chini ya Director Hanscana na imefanya vizuri Tanzania, leo anaweka bayana changamoto wanazopata wasanii wakiwa wachanga kwenye kupromote video zao yeye kama mmoja wa wasanii.

Video hii ya Gentriez na Director Hanscana unaweza kuipata kupitia show ya mziki bomba ya Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo (160).

Amesema haya kwenye exclusive, "Kwanza kabisa unajua kupeleka video kwenye TV sessions kwanza unatakiwa kujua muhusika wa kumpatia kazi yako ni nani laasivyo akipokea mtu hata hakujui anaweza hata asiangalie aipotezee kwasababu hujulikani."

Gentriez ameongelea pia video yake ya kwanza kutokufanya vizuri na ndio ilikuwa video nzuri kati ya video zake zote alizowahi kufanya kwasababu ya jina na pia location yeye kuwa kuishia Arusha mbali na sehemu anayopromotia video.

Msanii huyu alielezea, "So mara ya kwanza ilikuwa ngumu zaidi cause sikuwa na connections na video ikapotea hivihivi but this time namshukuru Mungu nnazo nna watu nawajua, anahusika nani na nampe nani kazi yangu."