Msanii Vanessa Mdee kutoka Tanzania

Mwanadada mrembo kutoka Tanzania Vanessa Mdee au akifahamika kama Vee Money mkali kwenye bongofleva ambae bado anatikisa kwa upande wa burudani kila siku na ngoma za ukweli makini.

Vanessa ameingia kwenye headlines baada ya kurudi tena na hit song mpya baada ya Niroge, iliyobeba title ya Cash Madame. Ameamua kuizungumzia single hii mpya na kusema ni ujumbe ambao ametoa kwa wanadada wote ambao ni tegemezi kwa wanaume.
 
 
Kupitia mtandao wa Instagram kwenye page yake Vanessa amezungumzia wimbo huo kwa kuandika haya:
 
"Wimbo huu ni tamko langu kwa wanadada zangu wanaojitegemea. Siku za kumtegemea mwanaume kwa namna yeyote ile zimepitwa na wakati. Afrika mpya inabidi ihamasishe wanawake wawe na mawazo huru ya kutomtegemea mwanaume. Nikiwa binti kama huyo, nimeangaliwa tofauti mara kadhaa, ila #CashMadame bila kuzingatia kazi yake wala mfuko wake, hatetereshwi na ana uhuru mkubwa!"
 
Ulikosa hitsong hii? Basi unaweza kuitazama sasa kwenye Mziki Fresh, Alhamisi saa 18:00 ndani ya chanel ya mziki za Afrika Mashariki TRACE Mziki (323). ‚Äč