A participant at Bongo Star Search

Shindano la kusaka vipaji vya muziki ambalo hufanyika kila mwaka la Bongo Star Search lilifanyika kwenye mkoa wa Arusha weekend iliyopita

Shindano la kusaka vipaji vya muziki ambalo hufanyika kila mwaka la Bongo Star Search lilifanyika kwenye mkoa wa Arusha weekend iliyopita kwa majaji kufanya mchujo wa kupata wa kuja Dar kushiriki.

Madame Rita Paulsen akiongozana na majaji wengine Salama Jabir na Master J walikutana na vituko vya aina mbalimbali lakini pia vipaji havikuachwa nyuma.

 

Vipaji vilikua vingi sana ambapo kwenye mchujo mkali wa kwanza ulitokea kupata watu 32 ambapo kwenye mchujo wa mwisho ambao ulikua mkali ukabakiza watu sita akiwemo msichana mmoja anaerap.

Kutana na msichana mwingine wa rap Vanessa Mdee, ambaye ameteuliwa kwenye MAMAs 2015 itakayopeperushwa live kwenye MTV Base siku ya Saturday 18 July saa 21:00. Pia usikose kumpigia kura hapa.

Kituko ambacho hakitosahaulika ni pale ambapo alijitokeza kijana aliyevaa tshirt kubwa aliyoibandika picha ya Wema Sepetu akiwa amemkumbatia huku akisisitiza kwamba amefanya mazoezi ya Taarab, Hip-Hop, kwaya na aina nyingine ya muziki so majaji ndio wamchagulie nini aimbe.

 

 

Kingine ambacho hakitosahaulika ni mzee mwenye umri wa miaka 67 aliyejitokeza akisema anaouwezo wa kuimba lakini hata hivyo hakupita kwenye mchujo.

 

Hakikisha umepatana majaji Blake Shelton, Pharrell Williams and Adam Levine kwa msimu mwingine wa kipindi maarufu The Voice Tuesday, 14 July saa 19:30 CAT katika M-Net channel 103.