Mwigizaji wa bongowood Kajala

Kajala atoa maoni yake kuhusu kudidimia kwa bongo movie baada ya kifo cha Kanumba

Ni zaidi ya miaka miwili sasa hivi toka afariki dunia mwigizaji maarufu wa Tanzania Steven Kanumba ambaye alikua kinara na aliweza kuvuka mipaka na kufanya makubwa kwa kipaji chake.

Aliifanya Tanzania ikajulikana katika nchi mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutengeneza uhusiano mzuri na waigizaji wa Ghana, Marekani na sehemu nyingine za dunia.

Kujua mengi kuhusu bongowood, tazama Inside Bongowood kila Alhamisi saa 16:30 kwenye Maisha Magic East.

Toka amefariki kumekuwa na maneno kwamba bongomovie imelala, maoni ya Kajala ni nini? Anasema, "Ni kweli toka Kanumba afariki na bongomovie pia imeshuka lakini haijafa."
 
"Tunatakiwa kukaza tu na kuyaenzi yale yote makubwa na mazuri aliyoifanyia bongomovie, alivuka mipaka na alikua mtu wa kuthubutu... tunahitaji kupita kwenye hizo njia," Kajala kaongezea.
 
Kajala anayo movie mpya inaitwa Pishu ambayo kaonyesha uwezo wake humo ndani, kama upo karibu na Maisha Magic East jiandae kukutana nae pia hata kwenye baadhi ya movie alizoshirikishwa.