Msanii wa bongofleva Bob Junior

Msanii wa bongo Bob Junior asema mengi kuhusu uhusiano wake na Diamond Platnumz.

Tarehe 1 May msanii wa bongofleva Bob Junior alikwenda kwenye Zari All White Party na kufanya maswali ya watu yawe mengi imekuaje mpaka akahudhuria sababu wanajua hakuwa kwenye uhusiano mzuri na Diamond Platnumz.

Nunua Explora yako leo, upate habari za mastaa wengine kwa clear picha ya High Definition kwenye E! News Jumatano saa 17:45 kwenye E! Entertainment (124).

Kwenye exclusive interview Bob amekiri kwamba ameamua kuachana na wapambe ambao kwa kiasi kikubwa ndio walikua wanamshauri vibaya na kwamba hawakuwa wanataka apatane na Diamond.

“Nilikua naumia sana moyoni kukataa kwenda Diamond anavyonialika, alinialika hata kwenye birthday yake lakini wapambe wakanizuia, nilikua natamani sana kwenda ila ndio hivyo tena, sasa hivi nimeachana nao ndio maana hata nilikwenda White Party,” Bob alisema.

Kwa sasa Bob amesema studio yake imeimarika zaidi na kwamba amemuandalia Diamond zawadi ambazo ni beats kwa hiyo anytime soon usishtuke ukisikia Bob Junior kafanya kazi tena na Diamond.

Bob Junior na Diamond walikaa bila kusemeshana kwa zaidi ya mwaka mmoja na nusu ambapo pamoja na kwamba Diamond ilifikia time akataka wapatane, Bob aliendelea kukaza sababu ya kushauriwa na wapambe.