Mwigizaji kutoka Tanzania Yusuph Mlela

Yusuph Mlela kafunguka juu ya Bifu lake na Hemed PHD

Kutana na muigizaji wa longtime kwenye  Bongo movies ambae pia ni mwanamitindo, director mkimfahamu kama Yusuph Mlela na mmiliki wa Mlela Production Tanzania pia ameigiza movie kama In The State of The Enemy, Makonda na kadhalika.

Ungana na waigizaji wengine kutoka Tanzania kama Mohamed Fungafunga kwenye bongo movie Kibuyu, Jumamosi, 8 Oktoba saa 21:00 kwenye Maisha Magic Bongo.

Yusuph amefunguka juu ya bifu lake la mda mrefu iliyokuwa kati yake na muigizaji mwenzake Hemed PHD ambapo ameleza kuwa sasahivi wako kwenye mahusiano mazuri na hawana ugomvi tena.
 
Yusuph Mlela alisema, "Yalienda mambo na Hemed lakini sahivi tushasolve. Unajua sisi ni watu wazima sahivi so sahivi ni mda wa kutafuta pesa sio tena mambo ya kijinga kijinga."
 
Yusuph alifunga kwa kusema, "'Sahivi Jamiii inataka kujua sisi tunamafanikio gani sasahivi pamoja na kujulikana kote hiyo ni challenge kwangu mimi so na focus na mambo yangu binafsi sina habari tena za mabifu."