Msanii wa RnB Ben Pol

Ben Pol na wenzake wasaidiwa na wavuvi baada ya ajali ya boti

Mwimbaji staa wa RnB Ben Pol amesema sababu za kuichukua life jacket iliyomuokoa kwenye ajali ya boti na kuipeleka nyumbani.

Kuburudika na muziki zingine za RnB, jiunge na msanii maarufu Ne-Yo atakayeperform live kwenye MTV Africa Music Awards kule Durban, itakayopeperushwa Jumamosi 18 July saa 21:00 CAT kwenye MTV Base.

Kwenye exclusive na dstv.com, Ben amesema baada ya kupona kwenye ajali ya boti ndogo ikitokea kwenye kisiwa cha Mbudya kuelekea Dar es Salaam, alikataa kuirudisha life jacket iliyomuokoa ili akaitunze nyumbani kwake.

Amesema ataitafutia hata sehemu ya kuitundika ili mradi aonyeshe kwamba ameithamini kwa kuokoa maisha yake baada ya kukaa akiwa anaelea baharini kwa zaidi ya saa moja bila kupata msaada wala kuona yeyote akipita.

 

 

Ben na wenzake ambao hawazidi kumi waliokolewa na boti ya wavuvi baada ya kukaa kwenye maji kwa muda mrefu huku abiria mmoja waliyekuwa nae akipotea kwa saa kadhaa mpaka kesho yake alipopatikana baada ya kuokolewa na wavuvi wengine.