Msanii kutoka Tanzania Ben Pol

Ben Pol adai kuwa msanii wakwanza kuiwezesha RnB kupigwa uwanjani

Mkali wa RnB kutokea Tanzania Ben Pol ni miongoni mwa wasanii wakali haswa kwenye game ya bongofleva kwa upande wa RnB ambaye kwa sasa hivi anatamba na hit single yake Moyo Mashine.

Kutana na Ben Pol ndani ya Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo.
 
Msanii huyu ameongelea swala zima la perfomance ya muziki wa R'n'b Tanzania kuwa huwa unakuwa perfomed ndani ya maukumbii tu lakini yeye ameitambulisha style ya tofauti na sasa unakuwa perfomed hata kwenye show za uwanjani.
 
Ben Pol aliongea haya, "Naweza kusema kuwa mimi ni msanii wa kwanza kuleta muziki wa RnB uwanjani, watu walishazoea wasanii wa RnB kufanya show ukumbini tu."
 
Aliendelea,"Kwa sasa wasanii wa RnB tunaweza kufanya show uwanjani mbele ya mashabiki zaidi ya elfu sitini hadi sabini ni kitu kikubwa. lakini kama sitakuwa msanii wa kwanza kufanya hivyo basi nitakuwa miongoni mwa wasanii waliofanya hilo likawezekana."
 
Ben Pol pia ameahidi kuachia kazi yake mpya baada ya Moyo Mashine siku si nyingi ili kufunga mwaka vizuri.