Bebe Cool

DStv yakutana na msanii wa Tanzania Bebe Cool na kafafanua ni kwa nini hasikilizi bongo

Ripota wako wa dstv.com Millard Ayo kutoka Dar es salaam nilikutana na mwimbaji staa wa Uganda Bebe Cool kwenye red carpet na nikaongea nae vitu vingi ikiwemo anavyoichukulia Bongo fleva kwa sasa.

Akaniambia siku hizi hasikilizi kabisa nyimbo za bongofleva kwa sababu hazina mvuto, hivyo kwenye playlist yake hakuna hata moja inatokea Tanzania.
 
Sio kwamba anauchukia muziki wa bongofleva bali muziki wa sasa haumpi hamu ya kusikiliza, anasema zamani ndio alikua anasikiliza sana bongofleva sababu mziki ulikua mziki kweli enzi hizo za kina Ay, Ray C, Proffesor Jay, Solothang, T.I.D na wengine.
 
Jiunge na wasanii wengine maarafu kutoka East Afrika kwenye Hitlist, Jumapili 23 August saa 11:00 kwenye Maisha Magic East.
 
Bebe Cool aliongezea kwa kusema msanii pekee ambaye amekua akimsikia sana na kumfahamu kwa sasa ni Diamond, na amemjua Diamond kwa sababu nyingi lakini sio kupitia muziki.
 
Unadhani Bebe Cool yuko sawa kusema bongofleva ya sasa sio kali kama ya zamani? Niachie comment yako hapa chini na itanifikia mtu wangu.