Msanii wa Tanzania Barnaba na Jose Chameleone wa Uganda

Baada ya kutoa single na Chameleone, sasa Barnaba adakua kilichoteka kwenye studio akiwa na Jose.

Bongofleva ya Novemba imepata ugeni mpya wa single mpya ya Barnaba ft. Jose Chameleone 'Nakutunza' ambapo kwenye hii post ya leo Barnaba ameshea na sisi kilichotokea studio akiwa na Jose.

Burudika na single hii mpya ya Nakutunza kwenye show ya muziki ya Mzooka kwenye Maisha Magic Bongo, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 CAT.
 
Anasema: "Jose Chameleone ni mtu yuko serious sana na anabadilika kwa dakika chache sana, dakika mbili mbele anaweza kuwa adui yako lakini yote hiyo ni sababu anaboresha kazi yake na anataka kuwa makini, anakuambia akitumia dakika 15 studio ni lazima zimlipe, hataki kupoteza muda."
 
Barnaba kaongezea: "Jose ni mtu ambaye pia kama mnafanya kazi pamoja lazima atake kukuridhisha wewe kwanza, ni mpaka useme yes kwanza ndio ataendelea... lazima ahakikishe ujio wake umekutendea haki."
 
Kingine kuhusu Jose Chameleone anachokisema Barnaba: "Mkikaa studio mkisema mnafanya kazi ni hatoki, tulikaa saa 16 studio na hatoki hata nje kunywa maji.... tulikaa ndani hakulala hata tone, mimi ndio nikawa nasinzia kwenye kochi na akawa ananiamsha yeye."
 
Kwa kumalizia, Barnaba amesema: "Kiukweli Jose Chameleone amenifundisha sana... ni legend, mwimbaji wa kimataifa ambaye nilitamani sana kufanya nae kazi toka siku nyingi, ameniongoza vizuri sana jinsi ya kufanya kazi inavyotakiwa."