Msanii Barnaba kutoka Tanzania

Barnaba ni miongoni mwa vocalist hatari Tanzania ambae sasa hivi ngoma yake kali inayohit ni Lover Boy.

Barnaba aliahidi kuitoa album yake aliyokuwa ameipa jina Nane Nane kwenye siku ya August 8 lakini aliahirisha baada ya sponsor wake wa album hiyo kubadilisha mawazo.
 
Kutana na Barnaba kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo.
 
Pia amezungumza kuwa imebidi aianze upya ili impe nguvu zaidi nakudai kuwa ushindani toka kwa wasanii wapya ni sababu za kujipanga upya.
 
“Vitu vingi nimebadili, kuna changamoto nyingi, majanki wanafanya vizuri sana, ukiruka huku unakutana na mashine kwahiyo inabidi kuwa makini, "Barnaba alisema
 
"Na mimi nikiwa kama mtu mzima, nafasi hizi za kuwa kwenye ubora nazihitaji, so I have to do something beautiful. Barnaba amedai kuwa siku ya Valentine’s atatoa bonus track ambayo huenda ikabeba jina la album hiyo," alimalizia.