Meneja wa Diamond Platnumz Babu Tale

Sina tatizo na Alikiba wala Meneja wake, Babu Tale kasema kwenye exclusive

Meneja wa Diamond Platnumz Babu Tale amekaa kwenye exclusive ya DStv na kuyaongea ambayo Watanzania hawayajui na hii ni baada ya kuonekana kwenye picha moja na Alikiba.

Babu Tale alishatolea ufafanuzi ile picha ambayo alipiga na Alikiba wakati wa futari na kusema wala hakuona shida kupiga naYe picha maana ni kitu cha kawaida na hakuna uadui kati yao, ni watu tu wanavyochukulia mambo.
 
Ungana na Diamond na Alikiba kupitia kipindi cha Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.
 
Tale amesema kilichopo kati ya Alikiba na Diamond ni ushindani wa kibiashara na sio kingine na hata yeye Tale ni rafiki mkubwa na meneja wa Alikiba.
 
Namnukuu akisema, "Meneja wa Alikiba hata kwenye birthday ya watoto wangu ni lazima awanunulie zawadi, hatuna tatizo la kibinadamu wala vita ni ushindani tu za kibiashara tu."
 
"Kelele za Alikiba na Diamond zimesaidia huu muziki uwe serious, kila mmoja sasa hivi anapigana kuhakikisha bidhaa yake inakuwa bora na kufikia viwango vinavyotakiwa, ushindani huu wa kibiashara kwangu ni mzuri na sio vita."