Diamond Platnumz

Mwimbaji Diamond Platnumz amesharudi nyumbani Tanzania kuendelea na harakati nyingine baada ya kufanya show kwenye miji tisa ya Ulaya ambapo yafuatayo ni mambo matano aliyoyasema.

1. Siwezi kutaja kiwango gani cha pesa ninalipwa nikienda kufanya show za nje kama Ulaya ila mapromota wa kule walikua wananitafuta siku nyingi sema hawakuwa na pesa za kutosha nikawa nakataa.
 
2. Pesa ambazo mapromota wa Ulaya walikua wanataka kumpa ni kuanzia milioni 4, 5 mpaka kumi na Diamond hakuwa tayari kwa hizo pesa ndio maana aliwaambia ni bora wasubiri baadaye waje kumpa pesa anayoitaka na awajazie ukumbi pale ambapo jina lake linakuwa limezidi kuwa kubwa zaidi.
 
3. "Safari yangu ya kwenda Ufaransa ilikua ni kutokana na mwaliko wa Fally Ipupa, kuna wimbo wake kanishirikisha... namshukuru sana kwa kunialika na familia yangu, kukutana kwangu na Awilo Ufaransa ilikua ni kifamilia tu, yeye ni rafiki wa familia."
 
4. Diamond amekiri pia reality show yake inaanza soon na itakua inaanzia kwenye internet alafu baadaye inaonekana kwenye TV japo hayuko tayari kusema itakua channeli gani.
 
Tukiingojea reality hii ya Diamond Platnumz, ungani na wapenzi wengine kwenye reality show ya Happily Ever After kila Jumatano saa 19:30 kwenye Maisha Magic East.
 
5. Mapromota wa nje nilikua nawakatalia kufanya show na mpaka sasa kuna nchi nyigine sijawahi kufika, nilikuwa nawaambia wanapesa ndogo sasa kama wanaona siwezi kujaza ukumbi niliwaambia wanisubirie tu mpaka nije kuweza kujaza wanipe hela nzuri.