Msanii wa bongofleva Chidi Benz

Tunaye rapper mahiri wa bongofleva kwenye hii post leo, ni Chidi Benz ambaye wiki zaidi ya tano zilizopita alikiri kwenye TV Interview kwamba utumiaji wa dawa za kulevya ulimuharibia.

Siku chache baadaye alichukuliwa na kupelekwa kwenye nyumba ya matibabu huko Bagamoyo Pwani ili aweze kuachana na utumiaji wa dawa hizo za kulevya na baada ya kutoka Rehab amekaa na ripota wa  DStv Millard Ayo na kuyasema yafuatayo.
 
Kutana na rapper huyu Chidi Benz kwenye show ya Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.
 
1. Haikua shida kwangu nilipokwenda kwenye nyumba ya matibabu, nilipokelewa vizuri na nilipewa huduma nzuri na kupata kila kitu nilichokua nahitaji kwa huo mwezi mmoja na zaidi.
 
2. Mimi sikutoroka kwenye nyumba ya matibabu kama ilivyoripotiwa, haikua kweli ni watu tu walisambaza lakini nilifurahi kuona wenye rehab walijitokeza kusawazisha.
 
3. Mambo ya madawa ya kulevya yalishapitaga na hata sitopenda tena kuulizwa kuhusu madawa kwenye Media, matibabu nilishamaliza na niko sawa.
 
4. Namshukuru sana meneja Babu Tale kwa kunipelekea nyumba ya matibabu, kama sio yeye inawezekana ningechelewa au nisingeenda kabisa, ila siku Maskani alikua ananiambia hata nikikupa pesa inawezekana nikaendelea kukuumiza zaidi.
 
5. Sisi wote ni binadamu ila watu wasihukumu sana kutokana na kile tunachokiona, wote tunafanya makosa kwenye haya maisha... kuhusu muziki Tale alinichukua akaniokota akanimwagia maji nikang'aa tena, yeye ndio namsikiliza atachoniambia mimi nafata.