Msanii wa Tanzania AY

Msanii wa Tanzania AY aongea kwenye exclusive na DStv kuhusu surprise yake

Mara yako ya mwisho kusikia ngoma kutoka kwa Ambwene Yessayah ilikua lini? Najua wenye kumbukumbu zao watasema ilikua juzijuzi tu hapa alivyoachia Zigo Remix ft. Diamond Platnumz.

Nani haipendi ngoma hii ya Zigo? Basi ungana na Diamond na AY tena kwenye Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.
 
Sawa, sasa kama wewe ni shabiki wa A.Y inabidi ukae tayari sababu soon atafanya kitu ambacho hajawahi kukifanya toka amezaliwa na toka aanze muziki vilevile.
 
A.Y amesema ataachia ngoma mbili kwa wakati mmoja very soon ambapo moja kafanya kolabo na nyingine kasimama mwenyewe.
 
Kwenye exclusive hii na DStv, A.Y amesema ngoma moja ya kolabo ndio hiyo kamshirikisha Joh Makini ambaye ni mshikaji wake au wamejuana toka mwaka 2004, lakini hawakuwahi kufanya ngoma pamoja.
 
A.Y amesema: "Najua watu wataipenda, nimeingia studio na Joh Makini na tumefanya kitu bora, ni mshkaji wangu wa kitambo hata tulikua tunajiuliza mbona hatujafanya ngoma mpaka sasa, yani watu waisubirie tu."
 
Mbali na muziki, A.Y pia unaweza kumpata kwenye Jikoni na Marion saa 17:00 Jumamosi kwenye Maisha Magic Bongo.