Mwigizaji Wema Sepetu

Inaonekana imekua ishu baada ya mwigizaji Wema Sepetu kupostiwa kwa mara ya kwanza kwenye Instagram ya mpenzi wake wa zamani ambaye ni Diamond Platnumz.

Toka walipoachana kulikua na kimya kirefu cha Diamond kumpost Wema lakini juzi alipompost na kusisitiza watu kujitokeza kwa wingi kwenye show ambayo imeandaliwa na Wema, Christian Bella na Idris Sultan, wengi wakafurahia na kumsifia Diamond.

Ukweli ni kwamba Wema anasema anachoamini ni utengano wao ulikua ukiongezewa chumvi au kuendeshwa sana sana na mashabiki, anaamini pia kuna wengi hawakupenda kuona wawili hawa wakipeana support hata kama walikua wameachana.

Wema anasema ilifikia time alikua pia anajifanya hazipendi nyimbo za Diamond ila kiukweli alikua anajidanganya tu maana moyo wake bado ulikua na love na nyimbo za Diamond. Anasema: "Nilianza kuwa shabiki wa Diamond hata kabla ya kuwa mpenzi wake."

Wapenda nyimbo za Diamond kama Wema Sepetu? Basi ungana naye kwenye kipindi cha Mzooka, Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.

Wema amemalizia kwa kusema anayo furaha kuona amani imerejea kati yao japokua haimaanishi kwamba wamerudiana kimapenzi, anapendelea hali iwe hivi kuliko ilivyokua awali.