Rapper kutoka Nigeria YCEE akiwa Tanzania

DStv.com inaye rapper kutoka Nigeria YCEE ambapo kwenye hii post anayazungumzia maswala matatu na ni kama ifuatayo.

Moja ni changamoto alizozipata kufanya collabo na wasanii wenzake kabla hajajulikana. Pili, ameelezea juu ya swala la kutoza gharama yoyote pale anapoombwa kufanya collabo na msanii yeyote. Na tatu ametaja msanii anaemkubali kutoka Tanzania.

Rapper huyu amelezea kabla hajatoka ilikuwa ngumu sana kuweza kufanya collabo na wasanii wengine. Namnukuu aliposema: "Nigeria ni nchi yenye watu wengi na kila siku wanaibuka wasanii wapya na wengi huwa hawafiki malengo kwa hiyo ukiwa hujulikani na ukaomba collabo na wasanii ambao wameshatoka kimziki hawawezi kukusikiliza kwa hiyo mpaka utoke na ujulikane ndo inaweza kuwa rahisi hata wao kukusikiliza."

Katika swala la pili alilozungumzia rapper huyu pia kuhusiana na kutoza gharama zozote kama ataombwa kufanya collabo na msanii mwingi nikimnukuu majibu yake haya: "Kwa keli inategemea kwa sababu hiyo ni biashara na unakuwa unatoa huduma ila zaidi naeza nkasema inategemeana na ukaribu nilio nao na msanii huyo lakini hata bure pia nafanya."

Pia YCEE amemtaja msanii anaemkubali kutoka Tanzania na amesema haya: "Nkiongelea kwa Tanzania ntamuongelea Diamond kwa sababu amekuwa msanii anaenivutia kwa kuwa mchapakazi, pia yeye kuwa mchezaji na muimbaji kwa wakati mmoja na katika kazi zake huwa anafanya vizuri sana kwakel napenda kazi zake sana."

Najua sisi pia twapenda kazi yake Diamond sana, basi kutana naye kwenye Mziki Hit 10 kila Jumamosi saa 12:00 kwenye channel mpya ya TRACE Mziki (323).