Trey Songz, Vanessa Mdee na Maphirosa kutoka Afrika Kusini kwenye Coke Studio Africa

Ni msimu mpya wa Coke Studio Africa ambayo umetajwa kuwa mkubwa zaidi kulingana na nchi kumi na moja zinazohusika. Mbali na wasanii kutoka Afrika, Coke Studio Afrika pia ilimualika msanii mkubwa wa RnB kutoka marekani Trey Songz aliyekuwa nchini Kenya wiki iliyopita.

Trey Songz akiungana na wasanii wengine wamerekodi wimbo utakaonyeshwa kwenye msimu huu mpya wa Coke Studio.

Waikumbuka collabo ya Alikiba na Ne-Yo?

Kati ya wasanii hawa ilikuwemo Mtanzania Vanessa Mdee, wengine wakiwa Nyashinski (Kenya), Neyma (Mozambique), Emtee (South Africa), Stonebwoy (Ghana), Yemi Alade (Nigeria), Rema Namakula (Uganda), Lij Michael (Ethiopia) na Serge Beynaud (Ivory Coast) wakifanya kazi na producer maarufu kutoka Afrika Kusini Maphirosa.

Vanessa alielezea furaha kufanya kazi na Trey Songz, “Ni experience kubwa kwa maisha yangu ya muziki ambayo sitosahau kwa sababu nimejifunza mambo mengi kwenye studio.”

Uliyaskia ya Vanessa, Trey Songz na Yemi Alade?

Mrembo huyu kutoka Tanzania alimshukuru Trey Songz kwa kuhamasisha vijana kutoka Afrika. Vanessa pia aligusia kidogo kuhusu album yake mpya ambayo amehusisha producer Maphorisa na kuahidi itakuwa kali sana.

Ukiingoja Coke Studio Africa itakayoanza rasmi tarehe 10 Oktoba, kutana na Vanessa Mdee kwenye show ya Mzooka Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo.