Msanii kutoka Tanzania Madee

Mitandao ya kijamii kwa sasa haichukuliwi poa tena kama zamani, unaweza kusema neno moja au mawili kwenye Facebook, Twitter ama Instagram alafu ukajikuta mikononi mwa polisi Tanzania.
 
Hivi karibuni Tanzania waliuwawa polisi wanane kwa mpigo, kila mmoja akasikitika na hata wengine kama msanii Madee kuandika kwenye Twitter akitoa pole kwa Watanzania na Waziri wa Mambo ya Ndani.
 
Mbali na haya, kutuna na msanii Madee kwenye Mzooka siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa 16:00 ndani ya Maisha Magic Bongo (160)

Baada ya tweet ya Madee akitoa pole, mmoja wa followers wake aliibuka na kuijibu kwa jazba na kumwambia Madee anatoa pole ya nini na kwamba wanapewa posho lakini majeshi mengine hawapewi, acha wafe.

Baada ya maneno hayo, polisi Mbeya wamethibitisha kwamba mtu huyo alikamatwa na kwamba wamemkabidhi kwa polisi Iringa maana ndio anakotokea hivyo sheria itafata mkondo wake.

Tanzania ya sasa inazo sheria pia ya mtandao ambayo tayari imeshatumika na kushuhudia watu kadhaa wakifikishwa mahakamani ikiwemo waliomtukana Rais au serikali na wengine walioandika habari za uongo.