Alikiba on Coke Studio Africa

Alikiba ndani ya Coke Studio Africa

Alikiba, msanii maarufu mwenye tuzo nyingi kutoka Bongo, amewasili jijini Nairobi kujiandaa na maandalizi ya Msimu mpya wa Coke Studio Africa. Kwenye Msimu huu wa tatu wa show kubwa ya muziki wa Africa  Mwanamuziki huyu anayetamba na nyimbo ya Mwana kwa sasa, ameungana na wasanii wengine kutoka Africa ambao nyimbo zao zinafanya vyema ndani na nje ya nchi zao.

Alikiba aliongoza kwenye Kilimanjaro Music Awards kwa kushinda tuzo sita kupitia kibao chake cha Mwana.

Usikose kutazama tuzo la MTV Africa Music Awards 2015 saa 21:00 CAT, Jumamosi 18 July kwenye MTV Base, ikipeperushwa kutoka mjini Durban.

Atashirikiana na mmoja kati ya wanamuziki wa kike wanao kuwa kwa kasi kimziki Afrika, Diva, mwenye makazi Kenya pamoja na Nigeria. Wawili hawa watafanya kolabo moja kali itakayoandaliwa na producer Owuor Arunga mwenye tuzo ya Grammy aliyeshirikiana na rapper bora kutoka Marekani Macklemore.

Video mpya ya Alikiba Chekecha Cheketua, imepokelewa vyema na kinapigwa sana kwenye TRACE Urban (DStv Channel 325).

Mwaka huu, Coke Studio imehusisha vipaji vikali kutoka Kenya, Tanzania, Mozambique, Nigeria na Uganda. Alikiba ataungana na wasanii wakubwa kutoka Afrika Mashariki kama Avril, Maurice Kirya, Juliana Kayomozi na Fid Q.

Ikiwa ni mara yake ya kwanza kwenye Coke Studio, Alikiba amesema haya, “Nadhani ni mahali ambapo naweza kuonyesha mashabiki wangu  jinsi nina uwezo wa kufanya kazi nzuri sana. Wataona jinsi ushirikiano  wangu na msanii  mwingine unaweza kuwa mzuri."

Tarajia kusikia nyimbo zake kama Chekecha Cheketua ikifanyika upya ikiwa na muundo mpya.

Hadi sasa, Alikiba amekuwa na mwaka wenye mafanikio makubwa katika muziki, ziara nchini Tanzania na Marekani, kwa sasa yupo Nairobi ambapo amekutana na mshindi wa Oscar Lupita Nyong'o. Wawili hawa watafanya kazi pamoja kama mabalozi wa mradi wa kutokomeza ujangili dhidi ya tembo barani Afrika.