Msanii wa bongofleva AliKiba

DStv yakutana na DStv ambapo anaongelea video yake anayoipenda zaidi.

Alikiba ambaye ni mwimbaji staa wa bongofleva mmiliki wa single ya Lupela ni miongoni mwa watu wanaoona au kujua michezo mingi ya mastaa kwenye kutengeneza headlines.

Patana na Alikiba kwenye show ya Mzooka saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo kila Jumatatu hadi Ijumaa.

Kwenye exclusive interview na DStv kupitia ripota Millard Ayo, Alikiba amesema kamwe hatokuja kutengeneza kiki bali kazi zake ndio zitampa kiki kwa watu kumzungumzia na kumkubali siku zote.

 
Ali anasema toka anaanza muziki tayari mashabiki zake wanajua hakuwa mtu wa kutengeneza kiki hivyo hakiwezi kuwa kitu atachopenda kukifanya japo anaamini kila mtu ana aina ya maisha yake anayoona ni sawa zaidi.
 
Pia ameongezea kwamba katika vitu huwa vinamsumbua sana ni pale anapotaka kutoa single mpya, kwa sababu anazo nyingi huwa inampa tabu kuipata moja ya kuachia ila huwa anahusisha watu mbalimbali ukiwemo uongozi wake.
 
Katika video zake zote Alikiba, anayoipenda zaidi ni Chekecha kwa sababu anaamini ubunifu uliotumika ni wa kipekee. Anasema, "Kiukweli ilikuja tofauti sometimes uelewa tu ndio unatofautiana na kila mtu aliipokea kivyake na huwa inatokea shabiki anatengeneza video yake kichwani pale msanii anapochelewa kufanya video."
 
Sisi twazipenda videdo zake zote, basi kutana na msanii huyu kwenye show ya Mzooka saa 16:00 kwenye Maisha Magic Bongo kila Jumatatu hadi Ijumaa.