Msanii wa bongofleva Ali Kiba

Ali Kiba asema haya baada ya kushinda Kilimanjaro Awards

Staa wa muziki wa bongofleva Ali Kiba amechukua headlines nzito weekend iliyopita baada ya jina lake kutajwa kwenye ushindi wa tuzo sita za Kilimanjaro Awards zilizotolewa nchini Tanzania.

Usikose kutazama tuzo lingine la BET Awards, ambaye mtanzania Millen Magese amewadiwa tuzo maalum, saa 20:10, Jumanne 30 June kwenye BET (129) na BET2 (135). Pia unaweza kuirekodi kwenye DStv Explora yako.

Baada ya ushindi huo, Kiba ambaye yuko Marekani ameyaandika haya maneno ili yawafikie mashabiki wake.

"Ningependa kuchukua nafasi hii kutoa shukrani zangu kwanza, kwa Mungu Muumba aliyenipa kipaji hiki, pili familia yangu kwa kuniongoza na kunipa moyo wa kufanya kazi zaidi, my management."

"Asante kwa kuniongoza vyema. Mashabiki wangu wa dhati asanteni sana kwa kuthamini kipaji changu na kupenda kazi zangu! Nawapenda na kuwashukuru from the bottom of my heart. Mungu awabariki sana ...#KingKiba."

Miongoni mwa mastaa waliojitokeza kumpongeza Kiba ni pamoja na warembo wawili ambao ni wapenzi wa zamani wa Diamond Platnumz, Jokate na Wema Sepetu.