Msanii kutoka Kenya Akothee

Kutana tena na msanii kutoka Kenya Akothee anaefanya vizuri kwenye game ya muziki kwa Afrika mashariki ambaye tayari ameshatunukiwa tuzo mbili.

Akothee anakujia na ngoma zake kama My Sweet Love kwenye Kenya 10 saa 20:00 ndani ya TRACE Mziki (323).

Mrembo huyu alitakiwa kufunga ndoa na mwenza wake raia wa Uswisi tarehe 5 Novemba mwaka huu lakini ndoa hiyo haikufanyika. Hii ni baada ya Akothee kubadilisha mawazo yake na kusema kuwa awezi kuendeshwa na mwanaume.

Pia uliyaskia ya Akothee na kiasi cha pesa anachotaka kulipwa kabla ya kufanya collabo na msanii yeyote?

Akothee alieleza kuwa mwanaume huyo alimkataza kuudhuria tuzo za Afrimma za Marekani ambapo aliibuka na tuzo ya Best Female Artist kwa Africa Mashariki.

Tunamnukuu, "Aliniambia nichague kati ya muziki na yeye na nimechagua muziki. Ni mimi na maamuzi yangu kwanza mwanaume hanipangii cha kuamua."

Akothee alimalizia, "Na siwezi kuhamia kwenye nyumba ya mwanaume, tukifunga ndoa yeye ndiye ahamie kwangu, siwezi kutulia na kitu kidogo mwanaume anatakiwa afit kwenye mipango yangu sio mimi kwenye mipango yake."