Afande Sele

Msanii Afande Sele anautaka ubunge

Ni msanii wa siku nyingi sana Tanzania ambaye aliwahi kuvishwa mpaka taji la mfalme wa rhymes, Afande Sele, na sasa anautaka Ubunge wa Morogoro Mjini.

Yeye na Profesa Jay wamekua miongoni mwa wasanii wa Tanzania ambao wameamua kujitokeza kugombea Ubunge kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Ukitaka kujua mengi kuhusu wasanii wakubwa Tanzania na maisha yao, usikose kuitazama kipindi cha majadiliana Mkasi kila Jumapili saa 16:00 EAT kwenye Maisha Magic Bongo.

Pamoja na yote hayo, mpaka sasa Afande hajazindua kampeni zake za Ubunge wa Morogoro mjini anaoutaka, sababu ni pesa kukosekana yani anashindwa kufanya kitu alichokitaka.

Amesema, "Nafahamika sana na ninaheshimika sana, wengi wanataka kuhudhuria mkutano wangu hivyo ni lazima niwe na sound ya uhakika kuwafikia watu, kadi, bendera na vitu vingine vya maana kukamilisha, vitu kama hivi kwenye chama changu ambacho hakina ruzuku vimekua ngumu kuvipata lasivyo tuchangishe michango."

"Kila kitu kimekua shida kwangu sasa hivi, ndio maana ninachelewa sababu nataka kufanya kampeni ambazo zinafanana na jina langu na heshima yangu pia nafasi yangu kwa jamii, kwahiyo najipanga ili nifanye kitu chenye mashiko," asema Afande.

Kwa kumalizia Afande amesema: "Mpaka sasa Morogoro mjini mimi ni mgombea ambaye nazungumziwa sana sababu nilikua na makundi ambayo yalikua yananisupport, nimekua mzalendo na pamoja na kupata umaarufu sikuwahi kuhama Morogoro, mimi ni mzalendo."