Abdu Kiba

Msanii wa bongofleva Abdu Kiba akaa chini na DStv kwenye interview

Abdu Kiba ni miongoni mwa mafundi wa kuandika nyimbo za bongofleva kwenye muziki wa sasa hivi ambapo leo anashare experience yake kidogo mapenzini.

Ukitaka kujua mengi kuhusu mapenzi, usikose kutazama Tujuane Plus kila Jumanne saa 19:30 kwenye Maisha Magic East.

Hajawahi kumfumania mpenzi wake na mwanaume mwingine lakini anaamini ikitokea hiyo bahati mbaya hatofanya chochote kama kumuadhibu yeyote kati ya wawili hao.
 
Kumekua na kesi nyingi kwenye nchi za Afrika ambapo wanaume huwapiga wake zao au wapenzi wao pale wanapowafumania, Abdu Kiba anasema haungi mkono hiyo kitu, kama mwanamke kakosea anasemeshwa tu alafu anaachwa lakini sio kumpiga.
 
Abdu Kiba ambaye ana single mpya sasa hivi inaitwa Ayayaa Ft. Ruby, amesema mapenzi ni uwanja mpana, kuna wasichana wengi tu hivyo mmoja akizingua haimaanishi umefikia mwisho wa maisha, tafuta mwingine mnaendana na usonge mbele.